Mwanamuziki Mkongwe Afande Sele Atoa Wito Huu Kwa Wasaniii - EDUSPORTSTZ

Latest

Mwanamuziki Mkongwe Afande Sele Atoa Wito Huu Kwa Wasaniii

 




Ameandika @afandesele1976 kupitia ukurasa wake wa Instagram.


"Kuna siku nilipigiwa simu na watu wa Cosota kwamba wanataka nipeleke nyimbo zangu zoote nilizowahi kurekodi kwenye maisha yangu ya muziki ili zikasajiliwe kisha niendelee kupokea mrahaba yaani malipo kutokana na nyimbo zangu..,🎤🪕


Baada ya taarifa hiyo tamu kutoka Cosota nikaanza kuorodhesha nyimbo zangu zote kuroka kwenye Albam zangu tano na baadhi ya nyimbo nilizotoa kama single nje ya Albam ambazo pia ni nyingi. Hapa mtihani ulikua ni mkubwa sana kwani baadhi ya nyimbo nilizisahau kabisa na baadhi nilizikumbuka lkn sikujua nitazipata wapi wakati huu?


Bichwa langu lilipotulia akili ikakumbuka kumpigia simu huyu ndugu yangu Ibra Nyange 'Mbavu'.. ambae siku zote najua huyu ni mmoja wa wafuasi wa mziki wangu sio shabiki wangu. Na kweli kupitia kwa huyu ndugu Mbavu nikapata nyimbo zangu zooooteeee kwa haraka na hakika...✍️


Wito wangu kwa wasanii wadogo zetu wajitahidi kufanya kazi zitakazo wapatia wafuasi sio mashabiki...Na wafuasi huja kutokana na Tungo zako sio mauno...poda wala pamba zako.. Sina Hatia 🙌






Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz