Mwakalebela Akubali Yaishe, Atangaza Rasmi Kutogombea Kwenye Uchaguzi Mkuu -Video-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest

Mwakalebela Akubali Yaishe, Atangaza Rasmi Kutogombea Kwenye Uchaguzi Mkuu -Video-Michezoni leo

Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Frederick Mwakalebela (kushoto).

 

MWANACHAMA mwandamizi na Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Frederick Mwakalebela ameweka wazi nia yake ya kutogombea nafasi yoyote ya uongozi ndani ya klabu hiyo, kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Julai 10, 2022

 

Mwakalebela alisema kuwa, dhamira yake kwa sasa sio kuchukua fomu kwenye uchaguzi huu wa siku za hivi karibuni, na kukili kuwa mafanikio yote wanayopata klabu hiyo kwa sasa, hawakuwa peke yao bali kuna baadhi ya watu waliwaunga mkono

 

“Mimi dhamira yangu haikuwa kuchukua fomu kwa msimu huu, tumeona jinsi tulivyopipokea timu katika kipindi kigumu na tumefika kipindi cha neema, hatuwezi kusema tumefika hapa peke yetu, kuna watu walikuwa nyuma kusaidia kufika pale.” Alisema Mwakalebela

 

Aidha kiongozi huyo mwandamizi aliendelea kusema kuwa, aliamua kuja klabuni hapo siku ya leo, ili kuwaaga rasmi wanachama na mashabiki wa timu hiyo kwa kuwa hatogombea tena kwenye uchaguzi huu, bali kwa sasa ataunga mkono jitihada za mhandisi Hersi Said ambayo amerudisha fomu ya nafasi ya urais.

 

“Mimi nimekuja kuaaga rasmi mashabki wa Yanga kwamba sitagombea na kuUnga mkono jitihada za Hersi kugombea urais kwa klabu yetu ya Yanga.” Alisitiza kiongozi huyo

 

Hersi alichukua fomu kimya kimya siku za hivi karibuni mara baada ya utaratibu huo kutangazwa na Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya klabu hiyo Wakili Mchungahela, na siku ya leo alirejesha fomu hiyo huku akisindikizwa na baadhi ya wanachama wa klabu hiyo.

 

Yanga inakwenda kufanya uchaguzi huo kwa mara ya kwanza, toka walipofanya mabadiliko ya katiba na hivyo cheo cha Mwenyekiti wa klabu hiyo kwa sasa nkitfahamika kama rais wa klabu.

The post Mwakalebela Akubali Yaishe, Atangaza Rasmi Kutogombea Kwenye Uchaguzi Mkuu -Video appeared first on Global Publishers.





Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz