BAADA ya mabosi wa Simba kukamilisha mazungumzo na Kocha wa APR ya Rwanda, Mohammed Erradi Adil raia wa Morocco, imebainika kuwa, mshahara wake ni mkubwa kuzidi wa aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Pablo Franco raia wa Hispania.
Inaelezwa kwamba, Erradi ndani ya APR, analipwa mshahara wa Euro 20,000 ambayo ni sawa shilingi milioni 50 za Kitanzania, wakati Pablo alikuwa akilipwa mshahara wa dola 13,000, takribani shilingi milioni 30 za Kitanzania.
Simba imeachana na Pablo kutokana na kushindwa kufikia malengo ya msimu huu kufuatia kupoteza makombe yote mawili ya Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho la Azam Sports, huku ikifeli kucheza nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika ikiishia robo fainali.
Baada ya Pablo kupewa mkono wa kweheri ndani ya Simba, uongozi wa klabu hiyo haraka umeanza mchakato wa kusaka kocha mwingine wa kuchukua mikoba ya Mhispania huyo.
Erradi alikuwepo hapa nchini baada ya kuitwa na mabosi wa Simba kwa ajili ya kufanya mazungumzo ya kujiunga na timu hiyo ambapo mazungumzo yao yalipokamilika, alirejea Rwanda kuendelea na majukumu yake.
Kitendo cha kocha huyo kufanya mazungumzo na mabosi wa Simba huku mwenyewe akikiri, kiliwapa presha APR kwa kuwa walikuwa hawajui kama tayari ameshamaliza na Simba kwani mkataba wake na APR upo ukingoni.
Taarifa za uhakika kutoka APR, zinasema kwamba, mabosi wa timu hiyo wameanza kutuliza presha ya kumpoteza kocha huyo baada ya kubaini mshahara anaotaka kulipwa na Simba ni mkubwa kumzidi Pablo.
“Ni kweli kocha amekiri kufanya mazungumzo na Simba na amewaambia ukweli kwamba haitokuwa rahisi kwa kuwa anahitaji mshahara mkubwa ambao ameikuwa akiupata Rwanda.
“Lakini hata viongozi wenyewe wameutafuta mshahara wa Pablo na kulinganisha na wao ambao wamekuwa wakimpa Erradi wamegundua itakuwa ngumu kwa Simba kufanikiwa kumlipa, hivyo kwa sasa wanaamini hawatoweza kumpata,” alisema mtoa taarifa kutoka APR.
STORI: IBRAHIM MUSSA
The post Mshahara Kocha Mpya Simba Kufuru, Amfunika Pablo, Ishu Yake Ipo Hivi… Soma Hapa appeared first on Global Publishers.
No comments:
Post a Comment