Mkubwa Fella Avunja Ukimya Kuvunjika Kundi la Yamoto Band "Walizengua Kila Mmoja Alijiona Mkubwa Kufanya Kazi Peke yake" - EDUSPORTSTZ

Latest

Mkubwa Fella Avunja Ukimya Kuvunjika Kundi la Yamoto Band "Walizengua Kila Mmoja Alijiona Mkubwa Kufanya Kazi Peke yake"


Mkurugenzi wa kituo cha kukuza vipaji cha Mkubwa na Wanawe na Meneje wa msanii Diamond Platnumz, @mkubwafellatmk amefunguka kuwa kama Yamoto Band (Ya akina Aslay) wangetulia basi wangekuwepo hadi leo kwenye Band hiyo,lakini wao ndio waliozingua. Mkubwa Fella amedai YB walizingua kwenye Ufanyaji kazi,kila mmoja aliona anaweza kufanya kazi kivyake na sio kama kundi tena na hatimaye kundi likafa.

Fella pia amefafanua kauli ya Diamond aliyoiweka kwenye insta story yake uwa ikitokea amefariki (Diamond), basi bendera ya Tanzania haitakuwepo kwenye list ya wasanii wa Afrika wenye ushawishi duniani, (List ni kwa mujibu wa mdau mmoja huko Twitter aliye tengeneza list yake ya wasanii wa Afrika wenye ushawishi Duniani).

Mkubwa Fella amedai Bongo Flava ina wasanii wengi wazuri ila Diamond amejua kujiongeza zaidi na kupambana kuliko wengine, hivyo kauli yake inawakumbusha wasanii wengine kuwa kufanya vizuri ndani na kuogelea na wanawake kwenye Madimbwi safari bado ndefu, njooni Tupambane.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz