Hawa Hapa Walimsafirisha Mtoto wa Mtaani Uingereza Ili Wamtoe Figo Wampe Mtoto wao Mgonjwa - EDUSPORTSTZ

Latest

Hawa Hapa Walimsafirisha Mtoto wa Mtaani Uingereza Ili Wamtoe Figo Wampe Mtoto wao Mgonjwa


Huyu ndio seneta na mke wake wanaotuhumiwa kula njama na kumpeleka kijana wa mtaani mwenye umri wa miaka 15 nchini Uingereza ili kumtoa figo na kumpa mtoto wao wa kike mwenye matatizo ya figo.

Wawili hao walikamatwa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Heathrow.

Seneta huyo alikutwa na pesa taslimu takribani shilingi milioni 58.

Nwanneka Ekweremadu (55) na Ike Ekweremadu (60) ni raia wa Nigeria. Ike amekuwa Mwanasiasa maarufu sana kwa miaka 19 na amewahi kushika wadhifa wa juu wa uongozi.

Mtoto ambaye alisafirishwa kwa ajili ya kutolewa viungo sasa yuko salama mikononi mwa polisi.

Kesi yao ilianza kusikilizwa jana na hivi sasa imeahirishwa hadi Julai 7 , wawili hao wamerudishwa rumande.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz