Mapya yaibuka Mke aliyepigwa Risasi Mwanza, Ushirikina watajw - EDUSPORTSTZ

Latest

Mapya yaibuka Mke aliyepigwa Risasi Mwanza, Ushirikina watajw






Rafiki wa pande zote mbili yaani Mume na Mke waliouwawa kwa tukio la Risasi Swalha Salum na Said Oswayo amefunguka mapya juu ya maisha ya wawili hao.

Akizungumza na Millard Ayo katika Msiba wa Swalha rafiki huyo aliyejitambulisha kwa jina la Hadija Ziota amesema Marehemu Swalha alikua mdogo wake na rafiki yake kipenzi na amefanya naye kazi kwa muda mrefu.

Amesema licha ya hivyo pia alikua na ukaribu na Marehemu Saidi aliyekua Mume wa Marehemu kwa kipindi kirefu na kifo chake kimemuumiza licha ya kuwa aliyoyafanya hayakua mazuri.

Alisema, yeye alihudhuria kwenye ndoa ya wawili hao na baada ya hapo ukaribu wao ulipungua kutokana na ubize wa kazi hivyo kupelekea kutojua vitu vilivyojiri hapo kati.

“Vitu vilivyokua vinaendelea kati yao hapo kati sivijui kabisa, lakini kuna siku moja nili view status nikaona Swalha ameposti njiwa, nikashangaa nikamuuliza hii imekaaje, akaniambia dada angu mambo ni mengi, ntakusimulia ntapita hapo ofisini kwako,” Alisema Hadija


 
Alisema kweli Swalha alienda, ofisini kwake na kumulezea kwa undani kuhusiana na suala la njiwa.

“Aliniambia dada Hadija yaani huwezi amini kuna watu wanatutafuta kabisa mimi na Mume wangu watuue sababu jana tumeamka asubuhi tukakuta pale uwani kuna njiwa wawili wamevishwa sanda akatoa simu yake akanionyesha wale njiwa alikua amewapiga picha,” Alifafanua hadija.



Hadija Ziota, Rafiki wa Pande zote mbili.
Alisema, Marehemu Swalha alimwambia binaadamu wabaya sana kwani kuna watu wanawatafuta wanataka wawaue.


Alisema, baada ya masuala hayo alimuuliza kama wako sawa na mumewe na Swalha alijibu kuwa hivyo hivyo tu ilimradi wanaishi sababu mumewe ni mkorofi anapenda kumpiga lakini mambo mengine wanavumiliana.

kuhusu Tabia ya Mwanaume Hadija amekiri ni kweli alikua mkorofi, mkali na mwenye wivu  sana na mkewe.

Kama ulipitwa;

Swalha Salum aliuawa kwa kupigwa risasi na mumewe kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

Swalha alipigwa risasi saba usiku wa Jumamosi Mei 28, 2022 na mumewe, Said Oswayo wakiwa nyumbani kwao katika mtaa wa Mbogamboga kata ya Busweru wilayani humo baada ya kuibuga ugomvi kati yao.


 
Siku mbili baada ya kutekeleza mauaji hayo huku juhudi za maofisa wa Jeshi la Polisi wakimtafuta, Jumatatu Mei 30,2022 mwili wa mtuhumiwa wa shambulio hilo, Said Oswayo nao ulionekana ukielea kwenye maji katika ufukwe wa Rock Beach jijini Mwanza huku ndugu wakithibitisha kuwa ni mwili wa ndugu yao.

Mwili wa Swalha umezikwa Jana mchana Mei 31 katika makaburi ya Kirumba baada ya kusomewa kisomo na kuswaliwa katika msikiti uliopo Kirumba mkoani humo huku siku rasmi ya mazishi ya mwili wa mmewe ukiwa bado haijajulikana.





Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz