elru87tYGBGEm Kocha Mpya Simba Kutangazwa Baada ya Siku 14, Baada ya Kuachana na Pablo Franco-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest

Kocha Mpya Simba Kutangazwa Baada ya Siku 14, Baada ya Kuachana na Pablo Franco-Michezoni leo

Wachezaji wa Simba wakifanya mazoezi.

 

UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa unatarajia kumaliza mchakato wa kupitia maombi na kumchagua kocha mpya wa kikosi hicho katika kipindi cha wiki mbili ambazo ni sawa na siku 14.

 

Simba Mei 31, mwaka huu walitangaza rasmi kufikia makubaliano ya kuachana na kocha wao, Pablo Franco na kocha wa viungo, Daniel Castro, kwa kile kilichoelezwa kuwa ni mwenendo usioridhisha wa kikosi hicho.

 

Taarifa hiyo pia iliweka wazi kuwa kikosi hicho kitakuwa chini ya kocha msaidizi Selemani Matola mpaka mwisho wa msimu.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally alisema: “Tangu tulipotangaza kuachana na aliyekuwa kocha wetu mkuu, Pablo Franco tumekuwa tunapokea wasifu (CV) za makocha mbalimbali kutokea nchi nyingi duniani ambao wanaonyesha nia ya kuhitaji nafasi ya kufundisha Simba.

 

“Tunatarajia kukamilisha mchakato huu wa kutafuta kocha mpya katika kipindi cha wiki mbili, ni mapema kwa sababu tunataka kocha mpya apate nafasi ya kufanya tathmini ya kikosi chake na kujua ni wapi anapoona mapungufu na anahitaji parekebishwe.”

CHAMA ATAJWA YANGA HUKO, KOCHA MPYA SIMBA AJA NA MIDO YA MPIRA | KROSI DONGO

The post Kocha Mpya Simba Kutangazwa Baada ya Siku 14, Baada ya Kuachana na Pablo Franco appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz