Viongozi Wizara ya Michezo Watembelea Kambi ya Twiga Stars-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest

Viongozi Wizara ya Michezo Watembelea Kambi ya Twiga Stars-Michezoni leo

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohammed Mchengerwa akiongea na wachezaji wa Serengeti Girls U17

VIONGOZI wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, wakiongozwa na Waziri Mohammed Mchengerwa, wametembelea kambi ya Timu ya Taifa ya Wanawake U17, Serengeti Girls, iliyopo Zanzibar, kuwatia motisha wachezaji hao kuelekea mchezo wao wa mwisho wa kufuzu kwenda Kombe la Dunia India dhidi ya Cameroun.

Katibu Mkuu Dkt Hassan Abbas

Akizungumza katika kikao na wachezaji hao, Waziri Mchengerwa amewataka kujitambua na kutimiza majukumu yao uwanjani kama walivyofanya ugenini ambako walishinda 4-1. Aliwapa ujumbe wa Rais Samia Suluhu Hassan, akisema Rais yuko pamoja nao.

 

Naye Naibu Waziri wa Michezo Pauline Gekul aliwataka mabinti hao kuzingatia maadili na ndihamu wakiwa kambini wakati huu wakielekea katika mechi hiyo.

Wachezaji wa Serengeti Girls wakisikiliza maelekezo kutoka kwa viongozi wa Wizara ya Utamaduni,Saaa na Michezo

Kwa upande wake Katibu Mkuu Dkt Hassan Abbas, alisema Serikali imeilea timu hiyo kwa kushirikiana na TFF tangu mwanzo na timu haina changamoto zozote huku akiwasomea aya vijana hao kutoka kwenye Quran Tukufu akiwataka wawe na subra na waelekeze nia zao katika jambo moja muhimu; nalo ni kushinda mechi hiyo na kufuzu kwenda Kombe la Dunia.

The post Viongozi Wizara ya Michezo Watembelea Kambi ya Twiga Stars appeared first on Global Publishers.





Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz