TANZANIA itafungua dimba na Sudan Kusini Juni 2 katika mchezo wa Kundi B Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge Uwanja wa FTC Njeru mjini Kampala, Uganda.
Mechi ya pili ya Twiga Stars itafuatia Juni 4 dhidi ya Ethiopia, kabla ya kukamilisha mechi za Kundi hilo Juni 6 kwa kumenyana na ndugu zao, Zanzibar hapo hapo FTC Njeru.
Nusu Fainali zitafuatia Juni 9 na Fainali pamoja na mechi ya kusaka mshindi wa tatu ni Juni 11 hapo hapo FTC Njeru.
No comments:
Post a Comment