Orlando Pirates Wafunguka "Ilitubidi Kumwaga Maji Kwenye Moto ili Kuuzima Kabla ya Kuanza kwa Mechi" - EDUSPORTSTZ

Latest

Orlando Pirates Wafunguka "Ilitubidi Kumwaga Maji Kwenye Moto ili Kuuzima Kabla ya Kuanza kwa Mechi"


Baada ya CAF kuipiga Simba SC. faini ya $ 10000 (Tsh. milioni 23) kwa kuwasha moto katikati ya uwanja wa Orlando Pirates nchini South Africa kitendo ambacho kilihusishwa na imani za kishirikina, Mitandao ya Nchi hiyo imeripoti kwamba tukio hilo lilianza kwa kutowapendeza Orlando Pirates wenyewe ambao waliwasilisha malalamiko yao haraka kwa Shirikisho hata kabla ya Wasimamizi wa mechi hiyo kupeleka ripoti.

“Wachezaji wa Simba SC waliwasha moto kwenye duara la katikati pale walipoanza huku wakijifanya wanaomba kabla ya mechi kuanza, ilitubidi kumwaga maji kwenye moto ili kuuzima kabla ya kuanza kwa mechi, mbali na malalamiko tulituma picha za tukio na kuonesha uharibifu uliotokea” taarifa ya Orlando Pirates ilisema.

"CAF imeikuta Simba na hatia ya kufanya matambiko hatari na kuwatoza faini ya R162,000 ($10,000), baada ya kusikiliza hoja za pande husika na kuzichambua video na picha zilizomo ndani yake, Bodi ya Nidhamu ya CAF imeamua kuweka vikwazo hivi kwa Simba kwa kushindwa kuzingatia na kutekeleza sheria zilizopo za usalama"

“Faini ya USD 10.000 kwa ajili ya kutekeleza matambiko hatari kwa Wachezaji wao kabla ya mechi kuanza, malipo ya pesa hizi lazima yafanywe ndani ya siku 60, vilevile Simba ina nafasi ya kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo ndani ya siku tatu" ——— CAF.




Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz