Kapombe, Manula Washusha Presha Simba, Ahmed Ally Afunguka Wapo Jumamosi-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest

Kapombe, Manula Washusha Presha Simba, Ahmed Ally Afunguka Wapo Jumamosi-Michezoni leo

Aishi Manula akiwa mazoezini.

 

MENEJA wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, amesema nyota wawili waliokuwa majeruhi katika kikosi chao, Aishi Manula na Shomari Kapombe, wameanza mazoezi rasmi kujiandaa kuikabili Yanga SC kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini hapa, Jumamosi hii.

 

Akizungumza na Spoti Xra, Ally alisema: “Tunaendelea na maandalizi yetu ambapo kwa sasa tunautumia Uwanja wa Gwambina kufanya mazoezi, kiukweli maandalizi yanaendelea vizuri na mkakati wetu ni kuhakiisha tunapata ushindi mbele ya Yanga.

Shomari Kapombe.

“Habari njema ni kwamba wachezaji wetu wawili ambao ni Shomari Kapombe aliyeumia nyama za paja tulipocheza dhidi ya Geita pamoja na Aishi Manula ambaye alikatwa na vioo kwenye vidole, wanaendelea vizuri na tayari wameanza mazoezi na wenzao, tunaamini kuelekea mchezo ujao watakuwa sehemu ya kikosi kitakachopambana na Yanga.”

STORI: JOHNSON JAMES, MWANZA

SAKATA la NTIBAZONKIZA na AMBUNDO KUFUKUZWA KAMBINI, YANGA Wamkataa REFA | KROSI DONGO..

The post Kapombe, Manula Washusha Presha Simba, Ahmed Ally Afunguka Wapo Jumamosi appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz