AC Milan washinda taji la Serie A kwa mara ya kwanza baada ya miaka 11 - EDUSPORTSTZ

Latest

AC Milan washinda taji la Serie A kwa mara ya kwanza baada ya miaka 11AC Milan walipepeta Sassuolo 3-0 na kushinda taji lao la 19 katika Ligi Kuu ya Italia (Serie A) kwa mara ya kwanza baada ya miaka 11.

Mashabiki wa Milan hawakufurahia kabisa uteuzi wa awali wa Stefano Pioli kuwa kocha wa kikosi hicho mnamo 2019 kwa misingi kwamba aliwahi kudhibiti mikoba ya watani wao, Inter Milan.

Ingawa hivyo, Pioli aliongoza Milan kutwaa taji la Serie A kwa alama 86, mbili zaidi kuliko nambari mbili Inter.

Olivier Giroud alifungia Milan mabao mawili huku jingine likijazwa wavuni na Franck Kessie.


 
Japo Inter walipepeta Sampdoria 3-0 katika siku ya mwisho ya kampeni za Serie A, ushindi huo wa masogora wa kocha Simone Inzaghi haukuweza kuzuia Milan kunyanyua taji.

Napoli waliambulia nafasi ya tatu baada ya kupepeta Spezia 3-0. Juventus nao walikamilisha kampeni zao za msimu huu ligini katika nafasi ya nne na hivyo kufuzu kwa soka ya Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) msimu ujao chini ya kocha Massimiliano Allegri aliyeshindia Milan taji la Serie A mnamo 2010-11.

Hadi walipotwaa ubingwa, Milan walikuwa wamejeribu kunyanyua taji la Serie A kwa zaidi ya miaka 10 bila mafanikio. Hata wanasoka wa zamani wa Serie A kama vile Clarence Seedorf, Filippo Inzaghi, Sinisa Mihajlovic, Vincenzo Montella na Gennaro Gattuso walijaribu kufufua makali ya Milan bila mafanikio.

Fowadi mzoefu raia wa Uswidi, Zlatan Ibrahimovic alikuwa sehemu ya kikosi kilichoshindia Milan ubingwa wa Serie A mnamo 2011. Akiwa na umri wa miaka 40, alitwaa taji hilo kwa mara ya pili mnamo Jumampili.

Kwa kushinda taji la Serie A akivalia jezi za Milan, kiungo Daniel Maldini alifuata nyayo za babake Paolo Maldini aliyenyanyua mataji saba ya Serie akichezea Milan, pamoja na babu yake, Cesare Maldini aliyeshindia miamba hao mataji manne ya Serie A.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz