Mwanamuziki Country Boy Afunguka Lebo yake ya Mziki Baada ya Kutoka Kwa Harmonize - EDUSPORTSTZ

Latest

Mwanamuziki Country Boy Afunguka Lebo yake ya Mziki Baada ya Kutoka Kwa Harmonize


Kwa sasa muziki wa Bongo fleva unakuwa kwa kasi sana kutokana na baadhi ya matukio ambayo tunaendelea kuyaona kunako muziki huu.

Miongoni mwa matukio yanayo tuonyesha ukuaji wa muziki huu ni kuchukuliwa kama ajira kwa vijana kwani muziki umekuwa msaada sana kwa vijana wengi Tanzania, na hilo analithibitisha rappa @countrywizzy_tz ambaye ameanzisha lebo yake mpya ya muziki kwaajili ya kuinua vipaji vingine ambavyo havijapata nafasi.

Country ameitangaza lebo hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo ameipa jina la @iam_music_co

Aidha, hatua hiyo inakuja ikiwa ni miezi mitatu imepita tangu aachane na Konde Music Worldwide.

"Kutokana na jitihada anazozionesha Rais wetu mpendwa, Mama yetu kipenzi MH SAMIA SULUHU HASSAN kuhakikisha Nchi yetu inasonga mbele mimi kama kijana sijataka kubaki nyuma Nimefungua kampuni iitwayo @iam_music_co ambayo itahusika katika kusaidia vijana mtaani ambao wengi wanatamani kutimiza ndoto zao lakini wanashindwa kutimiza kutokana na changamoto wanazokutana nazo.

Hivyo basi nakuja mbele yenu Watanzania na serikali kwa ujumla kuipokea KAMPUNI hii. Hatuna pesa nyingi lakini tunaamini katika kidogo tulichonacho kitatuvusha kutoka sehemu moja kwenda nyingne" - @countrywizzy_tz

✍️: @omaryramsey


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz