Morrison Apewa Kazi Maalum Kuimaliza Yanga Aprili 30 Kwa Mkapa, Mchezo wa Ligi Kuu-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest

Morrison Apewa Kazi Maalum Kuimaliza Yanga Aprili 30 Kwa Mkapa, Mchezo wa Ligi Kuu-Michezoni leo

Kiungo mshambuliaji wao Mghana, Bernard Morrison.

 

KUFUATIA kutokuwepo kwenye mipango ya mchezo wa marudiano wa robo fainali dhidi ya Orlando Pirates, benchi la ufundi la Simba limepanga kumuachia programu maalum kiungo mshambuliaji wao Mghana, Bernard Morrison kuhakikisha anakuwa sawa kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga utakaopigwa Aprili 30, mwaka huu.

 

Simba wanatarajia kuvaana na Orlando Jumapili hii katika mchezo wa mkondo wa pili wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, huku wakiwa na kumbukumbu nzuri ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa Jumapili iliyopita.

 

Katika mchezo huo wa Jumapili iliyopita, Morrison alihusika katika upatikanaji wa bao hilo la Simba baada ya kutengeneza penalti iliyofungwa na Shomari Kapombe.

 

Morrison anatarajiwa kuachwa kwenye msafara wa Simba utakaoenda Afrika Kusini kutokana na changamoto alizonazo na mamlaka ya uhamiaji ya nchi hiyo.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally alisema: “Kama ambavyo tulieleza hapo awali kuwa tunatarajia kumkosa Morrison katika mchezo wetu wa kule Afrika Kusini, lakini tunajua tutakuwa na mchezo muhimu dhidi ya Yanga tutakaporejea hivyo benchi la ufundi litaacha programu maalum ya utimamu wa mwili kwa ajili ya mchezo huyo na wote watakaosalia.  

STORI: JOEL THOMAS

The post Morrison Apewa Kazi Maalum Kuimaliza Yanga Aprili 30 Kwa Mkapa, Mchezo wa Ligi Kuu appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz