Liverpool Yaichakaza Man United, Ronaldo Apewa Dakika Moja ya Heshima-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest

Liverpool Yaichakaza Man United, Ronaldo Apewa Dakika Moja ya Heshima-Michezoni leo

Kiungo wa Liverpool Fabinho akigombea mpira na wachezaji wa Manchester United

KATIKA mchezo wa Ligi kuu nchini Uingereza uliochezwa kwenye uwanja wa Anfield klabu ya Liverpool imeibuka na ushindi mnono wa jumla ya mabao 4-0.

 

Mabao ya Liverpool yamefungwa na Luis Diaz aliyeanza kuzifumania nyavu mapema katika dakika ya 5 ya mchezo, Mohamed Salah alifunga mabao 2 katika dakika ya 22 na 84 na lile la mwisho likiwekwa kambani na Sadio Mane.

 

Kwa ushindi huo Liverpoo inakwea hadi nafasi ya kwanza ya msimamo wa ligi kuu nchini Uingereza ikiwa na jumla ya pointi 76 ikifuatiwa na Manchester City wenye pointi 74 wakiwa na mchezo mmoja mkononi.

Liverpoo inaongoza msimamo wa Ligi Kuu nchini Uingereza ikiwa na jumla ya pointi 76

Katika mchezo huo limetokea tukio la kiuana michezo katika dakika ya 7 baada ya mashabiki wa pande zote mbili wa Liverpool na Manchester United kusimama kwa muda wa sekunde 60 kwa ajili ya heshima kwa mshambuliaji wa Manchester United Cristiano Ronaldo aliyefiwa na mtoto wake mchanga wa kiume.

 

The post Liverpool Yaichakaza Man United, Ronaldo Apewa Dakika Moja ya Heshima appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz