elru87tYGBGEm Kocha wa Orlando Acharuka, Adai Klabu yake Haikustahili Kufungwa na Simba - EDUSPORTSTZ

Latest

Kocha wa Orlando Acharuka, Adai Klabu yake Haikustahili Kufungwa na Simba


Kocha wa Orlando Pirates Mandla Ncikazi amedai Simba inapaswa kuona aibu kwa ushindi ilioupata
KOCHA wa Orlando Pirates Mandla Ncikazi amesema klabu yake ya Orlando Pirates haikustahili kufungwa katika mchezo huo kutokana na kwamba Penati haikuwa sahihi kwa simba kupewa.

Mandla ameongea hayo wakati wa mahojiano na waandishi wa habari mara baada ya mchezo kumalizika, ametumia muda mwingi kuwalaumu waamuzi pamoja na kuhoji matumizi ya VAR kwani amedai kabla ya simba kupewa mkwaju wa penati nao pia walistahili kupata mkwaju wa penati.

Mchezo kati ya Simba SC na Orlando Pirates ulimalizika kwa Simba kuibuka na ushindi wa bao 1-0, bao lililowekwa kimiani na mlinzi wa kulia wa Klabu hiyo Shomari Kapombe.


                                          Mandla Ncikazi Kocha Mkuu wa klabu ya Orlando Pirates
Mchezo wa marudiano wa hatua hiyo ya robo fainali unatarajiwa kuchezwa Aprili 24 katika uwanja wa Orlando uliopo jijini Johannesburg Afrika Kusini ambapo klabu ya Simba itahitaji matokeo ya sare ya aina yoyote ile ili kuweza kufuzu katika hatua ya nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz