Kaizer Chiefs Yatangaza Rasmi Kuachana na Kocha wake Mkuu Stuart Baxter-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest

Kaizer Chiefs Yatangaza Rasmi Kuachana na Kocha wake Mkuu Stuart Baxter-Michezoni leo

Kocha wa Kaizer Chiefs aliyetimuliwa kazi Stuart Baxter

KLABU ya Kaizer Chiefs na Kocha Stuart Baxter wamefikia makubaliano ya pamoja ya kuvunja mkataba wa kocha huyo aiyerudi kuifundisha klabu hiyo kwa mara ya pili mara baada ya kuhudumu mwanzo kwenye klabu hiyo.

 

Akiwa na Kaizer Chief amefanikiwa kushinda michezo 9 ametoka sare michezo 6 na kufungwa michezo 8 na katika kipindi hicho klabu imefunga jumla ya mabao 25 huku ikiruhusu kufungwa mabao 23 kitendo ambacho kimepelekea mabosi wa Kaizer Chiefs kufikia makubaliano ya kuvunja mkataba wake.

Kocha wa zamani wa Kaizer Chiefs Stuart Baxter

Kocha Msaidizi Arthur Zwane pamoja na Dillon Sheppard watachukua mikoba hiyo hadi mwisho wa msimu huku mchezo unaofuata ukiwa ni dhidi ya Stellenbosch Jumamosi ya Aprili 23 mwaka huu.

 

 

The post Kaizer Chiefs Yatangaza Rasmi Kuachana na Kocha wake Mkuu Stuart Baxter appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz