Usipofanya Mazoezi Hiki Ndiyo Kitachokukuta - EDUSPORTSTZ

Latest

Usipofanya Mazoezi Hiki Ndiyo Kitachokukuta




Mazoezi ni kitu ambayo miili yetu huhitaji ili kujiimarisha, licha ya kuwa mlo ni muhimu sana pia mazoezi ni kitu muhimu sana kwa miili yetu. mwili huwa na tabia ya kutunza baadhi vimeng’enyo ambavyo ni glucose, protini, kabohaidreti na fati ambapo vina faida na hasara katika miili yetu hivyo basi inatakiwa vibalance na mazoezi ndio husaidia kubalance vimeng’enyo katika miili yetu.
kukosa mazoezi ni hatari kwa miili yetu kwakuwa husababisha mlundikano wa baadhi ya vimeng’enyo na kuuathiri mwili mfano fat au mafuta ambavyo vikirundikana ni tatizo mwilini pi sukari pia ikizidi na msala hupelekea ugonjwa hatari wa kisukari.

Leo nitazungumzia madhara ya kutofanya mazoezi ya mwili katika maisha yetu.

1: Uchovu mara kwa mara, mwili unapokosa mazoezi huchoka mara kwa mara na wakati mwingine bila hata ya kufanya kazi na hii ni kwasababu viungo hujibweteka kwa muda mrefu na kumfanya mtu kuwa na uchovu usioisha na kulala hali inayochochea uvivu kutokana na mafuta kujirundika.

2: Unene uliopitiliza na vitambi, kutokana na kukosa mazoezi humfanya mtu kujaa mafuta na nyama uzembe kwakuwa hachangamshi mwili wake ili kuyeyusha vitu hivyo.

3: Magonjwa ya moyo, kutokana na mwili kukaa tu hupeleke itilafu kwenye mzunguko wa damu na kufanya mwili kuanza kufeli kufanya kazi vizuri na hata kuathirika.

4: Kuharibu mfumo wa uzazi, hii ni kwa jinsia zote ambapo mwanaume anaweza kupoteza nguvu za kiume na ufanisi katika tendo vile vile mwanamke akapoteza mvuto ambapo hii huharibu mahusiano na ndoa nyingi kwa sababu ndogo tu ya kutofanya mazoezi.

5: Kifo, pia kwa kukosa mazoezi huweza mpelekea mtu hatari ya kifoo kwa kumsababishia matatizo mengi ya kiafya hata presha na kutokana na hilo mtu huweza fariki kabisa kutokana na magonjwa hayo ambayo kukosa mazoezi ndo kumeyaleta.
Kiujuma mazoezi ni muhimu tujitahidi kufanya mazoezi hata kidogo tu kulinda afya zetu na kuziboresha zaidi.




Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz