Paula Aanza Vijembe "Kwangu Habanduki Kwako Hatoboki…Jamani Wambeya Habari zenu Muwe na Siku Njema“ - EDUSPORTSTZ

Latest

Paula Aanza Vijembe "Kwangu Habanduki Kwako Hatoboki…Jamani Wambeya Habari zenu Muwe na Siku Njema“


PAULA Kajala @therealpaulahkajala ; ni binti wa mwigizaji wa Bongo Movies, Kajala Masanja au Frida na prodyuza wa Bongo Records, P Funk Majani ambaye kwa sasa yupo masomoni nchini Uturuki akisomea masomo ya uuguzi.


Paula amekuwa maarufu zaidi baada ya kujulikana anatoka kimapenzi na staa wa Bongo Fleva, Rayvanny @rayvanny akimpokonya Fayhma tonge mdomoni.


Amekuwa akiwarushia vijembe watu wanaomsakama kwamba alimchukulia Fayhma mtu wake ambapo safari hii amerusha kijembe kingine akimaanisha kwamba mwanaume wake hawezi kubanduka kwake.

Kupitia Insta Story yake, Paula ameandika; “Kwangu habanduki kwako hatoboki…jamani wambeya habari zenu muwe na siku njema. “
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz