Ukraine yafungua simu ya dharura kwa Waafrika wanaokimbia vita - EDUSPORTSTZ

Latest

Ukraine yafungua simu ya dharura kwa Waafrika wanaokimbia vitaSerikali ya Ukraine imeanzisha simu ya dharura kwa Waafrika na raia wa Asia wanaokimbia uvamizi wa Urusi, kulingana na waziri wa mambo ya nje.

Hatua hii inakuja kufuatia madai yaliyoenea ya ubaguzi wa rangi yanayowakabili waafrika wanaojaribu kuondoka nchini humo.

Wanafunzi wengi kutoka Afrika nchini Ukraine wameshirikisha simulizi za wao kuzuiwa na afisa wa usalama wa Ukraine kuondoka nchini humo.

Katika ujumbe wake wa Twitter, Waziri wa Mambo ya nje Dmytro Kuleba alisema mamlaka "zinafanya kazi kwa bidii" kuhakikisha usalama na kupita kwa wanafunzi wa Kiafrika na Asia.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz