Kisa Wachambuzi..Karia Avunja Ukimya...Awapa Makavu Live Kwa Kuhoji Kuhusu Waamuzi... - EDUSPORTSTZ

Latest

Kisa Wachambuzi..Karia Avunja Ukimya...Awapa Makavu Live Kwa Kuhoji Kuhusu Waamuzi...
Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF, Wallace Karia kwenye semina iliyofanyika jana, amesema kuwa katika watu ambao hawautendei haki mpira wa Tanzania ni Wachambuzi wa mpira, wanaongea sana mpaka wanatoka nje ya mstari na kuharibu mpira.
"Kuna wanaojiita Wachambuzi, sijui uchambuzi wamesomea wapi. Kusema ukweli katika watu ambao hawautendei haki mpira wetu ni Wachambuzi, wao wanasikilizwa na watu halafu wanatoa maoni yao binafsi".

"Mimi naona wao (wachambuzi) ndiyo wakati mwingine wanaopotosha na kuzua taharuki".

"Wenzetu Wachambuzi au waandishi uliopo hapa (kwenye semina) mkitoka muwe mmebadilika, siyo mechi imeisha unamuuliza Kocha aliyefungwa goli tatu kwamba mwamuzi kachezesha vipi". Amesema Rais wa TFF.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz