Smollett Aliyekuwa SHOGA Kwenye Series ya Empire atupwa Jela kwa Kudanganya Polisi - EDUSPORTSTZ

Latest

Smollett Aliyekuwa SHOGA Kwenye Series ya Empire atupwa Jela kwa Kudanganya PolisiMwigizaji Jussie Smollett kutoka nchini Marekani amesimama na kusema Mahakamani kwamba hana hatia baada ya mahakama kumtia hatiani na kumhukumu kifungo cha siku 150 jela.

Mahakama imemtia hatiani mwigizaji huyo aliyeigiza kwenye tamthilia ya Empire kwa makosa ya kudanganya polisi kwamba ni mwathirika wa shambulio la chuki na ubaguzi wa rangi.

Aidha, kifungo hicho kinahusisha miezi 30 ya kuwa chini ya uangalizi pamoja na shilingi milioni 335 ya faini na hasara iliyopatikana.

Baada ya hukumu hiyo kutolewa, Smollett ambaye ana miaka 39 amesisitiza kwamba hakudanganya katik taarifa aliyoitoa miaka mitatu iliyopita kwamba alishambuliwa na watu wawili.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz