Kwenye 5 Bora ya Wasanii Wenye TUZO Nyingi Barani Africa...CNN Wamtaja Namba Tatu - EDUSPORTSTZ

Latest

Kwenye 5 Bora ya Wasanii Wenye TUZO Nyingi Barani Africa...CNN Wamtaja Namba Tatu
Mjadala mkubwa unaoendelea kwenye Social Networks hivi sasa, ni kuwa Diamond si miongoni mwa wasanii watatu wakubwa barani Afrika, Hizi research au mitazamo hufanywa na watu kulingana na namba na mafanikio ya msanii husika na sometimes kwa mwaka husika pia,ni kazi ya msanii mwenyewe kumantain.

Kwa Diamond inawezekana hasiwe na impact kubwa barani Afrika kote kwasababu moja kuu,ametengeneza utajiri mkubwa wa mashabiki ukanda wa Afrika Mashariki na kati,hawa watu wamempatia followers,subscribers na hata streams kwa kiasi kikubwa, kwahiyo ukimuweka kwenye mafanikio ya Namba,basi atapambana vizuri na wasanii wengine tunao waona wao ndio wanastahili kuwa wasanii wakubwa Afrika.

Kimafanikio, Diamond kafanikiwa kwa kiasi kikubwa sana,ni miongoni mwa wasanii watano bora wenye tuzo nyingi barani Afrika,muziki wake umeenda mbali zaidi,na amekuwa nominated/Winner kwenye tuzo kubwa duniani kama MTV EMA, BET, n.k, unaanzaje kumpuuza msanii huyu?

2019 CNN walimtaja Diamond kama msanii namba 3 kwa ukubwa barani Afrika, nyuma ya Burna Boy, na mwanamama Angelique Kidjo. Lakini pia ametajwa na vyanzo vingi kwenye top 3 ya wasanii wakubwa Barani Afrika.

Aya tawanyikaaaa
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz