Kocha Azam Aapa Kutibua Ubingwa Yanga - EDUSPORTSTZ

Latest

Kocha Azam Aapa Kutibua Ubingwa YangaBAADA ya Jumatano kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 ugenini dhidi ya Namungo, Kocha Mkuu wa Azam, Abdul Hamid Moallin, ameweka wazi kuwa amefurahishwa na ari na upambanaji wa mastaa wa kikosi hicho na kuapa kuwa anataka kuona wanaendeleza hilo katika kila mchezo, hususani mchezo wao ujao dhidi ya Yanga.

Azam ambayo ilicheza michezo mitatu mfululizo bila matokeo ya ushindi, juzi Jumatano walitoka nyuma kwa bao 1-0 na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Namungo, ushindi ambao umewafanya wapande hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo na pointi 28 walizokusanya kwenye michezo 18.

Baada ya ushindi huo, Azam sasa wanajipanga kuvaana na Yanga ambao wanaonekana kudhamiria kushinda ubingwa msimu huu katika mchezo wao ujao wa ligi kuu, uliopangwa kuchezwa Aprili 6, mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Kocha Moallin alisema: “Kwanza kabisa nawapongeza sana wachezaji wangu kwa namna ambavyo walipambana katika mchezo wetu uliopita dhidi ya Namungo, ni wazi ulikuwa mchezo mgumu sana kwetu, nadhani tulikuwa tunakosa upambanaji wa namna hii kwenye michezo yetu iliyopita.


 
“Ninaitaka Azam ninayoifundisha mimi icheze kwa kiwango hiki kwa kila mchezo ulio mbele yetu hususan mchezo dhidi ya Yanga ambao najua ni mchezo mkubwa, lazima tuhakikishe tunatumia faida ya kucheza nyumbani kupata matokeo dhidi yao.”
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz