ELIZABETH Michael almaarufu Lulu Afunguka Issue ya Kumnyonyesha Mwanae - EDUSPORTSTZ

Latest

ELIZABETH Michael almaarufu Lulu Afunguka Issue ya Kumnyonyesha Mwanae


ELIZABETH Michael almaarufu Lulu au Mama G; ni supastaa filamu za Kibongo tangu akiwa na umri wa miaka mitano ambaye mwaka jana alijaaliwa mwanawe wa kwanza kwa mumewe, Francis Ciza almaafu DJ Majizzo.

Lulu au Lizy anasema kuwa, baada ya Mungu kumjaalia mtoto huyo aliyempa jina la Genesis atamnyonyesha hadi afikishe umri wa mwisho wa kumuachisha nyonyo na siyo kumuachisha tu, kisa kutaka usichana.

Akizungumza na Gazeti la IJUMAA, Lulu anasema kuwa, mastaa wengi wanaogopa kunyonyesha wakihofia maumbo yao kuharibika, lakini kwa upande wake hakuna cha kuhofia kwa sababu anatafuta afya njema kwa mtoto wake na siyo kitu kingine.

“Nitamnyonyesha hadi inapotakiwa, mambo ya kuhofia mwili wangu kuharibika siyo kweli kabisa, watu wanyonyeshe, mimi mambo ya kujihofia mwili wangu sitaki kwa sababu ukweli ni kwamba mimi ni mama na hakuna cha kubadilisha,” anasema Lulu.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz