Waliokuwa Wanasanii Lakini Wakangara na Kwenye Siasa - EDUSPORTSTZ

Latest

Waliokuwa Wanasanii Lakini Wakangara na Kwenye Siasa


SUGU.
Joseph Mbilinyi "Sugu" ni Mwana Hip Hop maarufu Bongo. Alianza muziki kama sehemu ya kujitetea na hali yake duni kimaisha. Sanaa haikumwangusha, ikampa umaarufu kutokana na nyimbo kali alizotoa. Mtaji wa watu alioupata kwenye sanaa akautumia kunyakua Jimbo la Mbeya Mjini katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

PROFESSOR J.
Ukirudi nyuma miaka ya 90 na 2000 utakutana na nyimbo za msanii Joseph Haule ‘'Prof.Jay" zilizokuwa moto wa kuotea mbali. Sauti ya Prof. Jay iliposikika watu walipagawa. Album kama "Machozi Jasho na Damu" vijana hawakuambiwa kitu zaidi ya kuipenda. Umaarufu wa sanaa alioupata Prof. Jay ndiyo uliokuwa mtaji wake hadi kuwa Mbunge wa Jimbo la Mikumi.

MARTHA MLATA.
Nyota yake ilianza kung’ara katika sanaa, zamani akiimba zaidi nyimbo za dini, baadaye alitumia umaarufu alioupata kwenye sanaa kuingia kwenye siasa, ambapo hakukwama kuupata Ubunge wa Viti Maalum CCM kutoka Mkoa wa Singida na baadaye kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi wa mkoa.

JOKATE MWEGELO.
Awali alipitia kwenye mashindano ya urembo, akashiriki Shindano la Miss Tanzania 2006 na kushika namba 2, umaarufu wake ukaanza kuchipuka. Hakuishia hapo, akajitosa kwenye muziki na filamu. Fani hizo zikazidi kumpa nguvu na ndipo alipoingia kwenye siasa ndani ya CCM akatumika kama mhamasishaji vijana, alipokubalika huko, Aliyekuwa Rais na mwenyekiti wa chama, Hayati John Pombe Magufuli akamteua kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe.

MKUBWA FELLA
Wengi wamemfahamu Said Fella kupitia muziki na hasa uongozi wa Kundi la TMK Wanaume Family. Miaka yote amekuwa mtu wa sanaa, hata kama haimbi lakini ni muhimili wa wasanii wengi, hiki ndicho ‘kinachombeba’ kwenye jamii. Mwaka 2015, aligombea Udiwani Kata ya Kilungule jijini Dar akashinda, lakini kilichomsaidia kuvuka ni umaarufu alioupata kwenye sanaa.

IRENE UWOYA
Alishika nafasi ya kwanza kura za maoni viti maalum mkoani Tabora kuwakilisha vijana ndani ya CCM, hakuwa mbunge kwa sababu kura za urais hazikumpa sifa, lakini mafanikio haya aliyapata baada ya kuutumia mtaji wa watu alioukusanya kutoka kwenye mashindano ya Miss Tanzania 2006 aliposhika nafasi ya 3.


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz