TCRA yatoa sababu bando kwisha haraka - EDUSPORTSTZ

Latest

TCRA yatoa sababu bando kwisha haraka



MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema kuongezeka kwa mitandao ya simu na kasi ya simu janja nchini ni miongoni mwa mambo yanayochangia ‘bando’ kwisha haraka. 

Mkurugenzi wa Masuala ya Sekta wa TCRA, Dk. Emmanuel Manasseh, aliyasema hayo jana mkoani Dar es Salaam, wakati wa mkutano wake na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF).

Alitaja mambo mengine yanayosababisha kumaliza 'bando' kwa haraka kuwa ni kuongezeka kwa kasi ya mtandao kwenye simu janja mfano kutoka 3G hadi 4G.

Mambo mengine, kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo ni ubora wa video na picha unavyoongezeka unasababisha matumizi nayo kuongezeka.

"Tuna “application” mbalimbali kwenye whatssap zinafanyiwa ‘update’ mara kwa mara nazo zinatumia data. Watumiaji wengi wa simu kuna vitu vinaendelea kwenye simu yake lakini mtumiaji hajui. Uwapo wa ‘application’ nyingi, zingine hazitumii hivyo zinamaliza ‘bando’,” alisema.


 
Alisema mamlaka hiyo imekuwa ikifanya majaribio mbalimbali ili kuhakikisha watoa huduma wanatoa huduma sawa na walichowaahidi watumiaji.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dk. Jabiri Bakari, alisema asilimia 27 ya watumiaji wa simu janja nchini ndio wanaonekana kutumia muda mdogo kusoma habari ndefu, hivyo wengi wanaotumia simu hizo hupoteza data bila kujua.

Alisema Tanzania inaongoza kwa kuwa na 'bundle' rahisi na salama Afrika na duniani, hivyo kila mtoa huhuma ana uwezo wa kubadilisha vifurushi kila baada ya siku 90.


“Utafiti mbalimbali duniani unaonyesha kuwa gharama za kupiga simu kutoka mtandao mmoja kwenda mwingine nchini Tanzania, ziko chini tofauti na nchi nyingine duniani, gharama za kawaida bila kujiunga na kifurushi, pamoja na gharama zilizounganishwa na kifurushi nazo zimeshuka, “ alisema.

Dk. Jabiri alisema kabla vifurushi havijabadilishwa, mtoa huduma  hupeleka  mapendekezo yake TCRA kwa ajili ya  kuangalia  kama vinaendana na utafiti uliofanyika ili kutomuumiza mlaji au mtumiaji wa huduma za mawasiliano nchini.




Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz