Shalo Mwamba, Mpoto na Sarafina Kimenoga Dubai.... - EDUSPORTSTZ

Latest

Shalo Mwamba, Mpoto na Sarafina Kimenoga Dubai....


Wasanii kutoka Tanzania, Sholo Mwamba na Sarafina leo wameutambulisha muziki wa Tanzania katika jukwaa jingine la
kimataifa walipofanya shoo kwenye ukumbi wa Sea Plaza katikati ya eneo la Dubai Expo.

Watu wa mataifa mbalimbali wakiwa wamesubiria shoo hiyo iloyochelewa kuanza kwa sababu za kiufundi, Sarafina ndiye alikuwa wa kwanza kupanda stejini na kuimba na kucheza huku akiwashirikisha mashabiki kutoka mataifa mbalimbali kwa kuimba huku akiwaeleza kisa cha hadithi ya kila wimbo aliouimba.

Safari ya kuitangaza Tanzania ilikolea zaidi alipopanda stejini msanii wa Singeli Sholo Mwamba na kuonekana kuwachezesha watu wa mataifa mbalimbali.

“Tumekuja hapa Dubai kutumia sanaa na utamaduni wetu kuitangaza Tanzania. Leo dunia imejua Tanzania kuna singeli na kuna muziki mzuri, usiku huu Sarafina amepata shoo nyingine katika ukumbi wa Earth Stage na kesho kazi inaendelea ukumbi mwingine uitwao Sun Stage ambapo Sholo Mwamba na Mrisho Mpoto watafanya shoo nyingine kubwa.

Ni wiki ya sanaa na utamaduni wa Tanzania kwenda “mtaa kwa mtaa” hapa Dubai na “mtaa kwa mtaa” katika kujitangaza duniani,” alisema Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi, aliyeshuhudia shoo hiyo hapa Dubai, UAE.


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz