Mange Kimambi Afunguka "Msameheni tu Diamond, Yeye na Team yake Hawakujua Maana ya Ile Bendera Ila Ajipange" - EDUSPORTSTZ

Latest

Mange Kimambi Afunguka "Msameheni tu Diamond, Yeye na Team yake Hawakujua Maana ya Ile Bendera Ila Ajipange"


Ameandika Mange Kimambi

"Naona wengi mmetaka ni -address hili swala la confederate flag kwenye video mpya ya Diamond, mi naona tumsamehe tu. Mi nimemuonea huruma tu maana nimeona ni kwamba tu hakujua maana ya hiyo confederate flag. Unless kama mtu alisoma historia ya utumwa especially kwa upande wa marekani au unless ana exposure sidhani kama anaweza kujua hii bendera ina maana gani. Obviously hata wanaomzunguka hawana exposure vile vile kwa hiyo hakuna aliejua maana ya hiyo bendera.

Ila kuna siku lazma atajikuta anaulizwa kuhusu hili akiwa nchi za nje hususan marekani. Maana marekani hawana mchezo kabisa kwenye swala la hii bendera. So cha kufanya ni ajipange tu siku akiulizwa atajibu nini, maana kama kuna siku atafanya interview marekani piga ua hii issue lazma watamkalia nayo kooni mpaka aombe msamaha . Hawatomwelewa mpaka aombe msamaha. Wamarekani weusi wako too sensitive na issue ya hii bendera…

Ila kwa sisi watanzania tumsamehe tu maana naamini kama angejua maana yake asingeitumia.

Kwa historia fupi tu, hiyo bendera ilikuwa ni bendera ya mikoa ambayo iliamua kujitoa kwenye nchi ya Marekani na kujiunga kuwa nchi ili waweze kuendelea na utumwa. Hii mikoa ilikuwa ni kusini mwa Marekani ambapo mikoa hii ilikuwa inategemea kilimo cha pamba, kilimo hicho kilikuwa kinafanywa na watumwa kutoka Africa. Sasa marekani kama nchi ilipopitishia sheria ya kukataza utumwa mikoa hiyo iligoma kukubali utumwa uishe kwa hiyo waakamua kujitoa kwenye nchi ya marekani ili waweze kuendelea na utumwa.Mikoa hiyo ilikuwa ni kama Atlanta, Mississippi, Alabama, Texas etc. So kukawa na vita kati ya mikoa hii na jeshi la Marekani na wakashindwa vita hiyo. Sasa hiyo mikoa iliyotaka utumwa uendelee hii ndio ilikuwa bendera yao.Kwa hiyo kwa wamarekani weusi hii bendera kwao inawakumbusha wazungu ambao waliendelea kung’ang’ania utumwa uendelee kiasi cha kutaka kujitoa kwenye nchi ya Marekani.Na mpaka leo hii wazungu wale ambao hawaogopi kujionyesha wao ni wabaguzi wa rangi huwa wanapeperusha bendera hii ili kuboa watu. Hakuna mtu mweusi mwenye akili timamu anaeweza kupiga picha na hii bendera. Kwa wamarekani weusi ni bora hata mtu apige picha na ile sign ya Nazi (Hitler) kuliko hii bendera" Mange
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz