Mwanaume Mweye Upara Akatwa Kichwa Wakiamini Kina Dhahabu - EDUSPORTSTZ

Latest

Mwanaume Mweye Upara Akatwa Kichwa Wakiamini Kina DhahabuPolisi nchini Msumbiji wanasema kichwa cha mwanaume mmoja mwenye upara kimekatwa na kuondolewa na wahalifu waliotaka kukiuza kwa mteja wao nchini Mali wakiamini kuwa kina madini ya dhahabu.

Imeelezwa kuwa, mteja wao alitoweka hivyo biashara yao ikabuma na kuamua kukitelekeza kichwa hicho katika mji wa kati wa Muandiwa.

Baadhi ya watu wa Msumbiji wanaamini ushirikina kuwa kichwa cha mwanaume mwenye upara huwa kina dhahabu ndani yake. Ripoti ya kwanza kuhusu kuuawa kwa wanaume wenye upara kwa ajili ya kuchukua vichwa vyao ziliripotiwa mwaka 2017.

Biashara ya viungo vya binadamu ni jambo la kawaida katika nchi za Msumbiji, Malawi na Tanzania ambako vinaaminiwa kuleta utajiri na bahati katika mapenzi. Sehemu za miili ya watu wenye ulemavu wa ngozi (ualbino) huuzwa kwa bei ghali.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz