Kwanini Wasanii wa Bongo Hawafiki Mbali..Hizi Hapa Sababu - EDUSPORTSTZ

Latest

Kwanini Wasanii wa Bongo Hawafiki Mbali..Hizi Hapa Sababu


Tunaona namna ambavyo wasanii wa Nigeria wanazidi kusonga mbele, Wizkid anatisha sana, Fireboy Dml sio mchezo, Burnaboy ndio Usiseme.

Sasa Kwanini Wasanii wa bongo hawafiki mbali? kila siku Diamond tu. kiukweli Nimetafakari sana lakini nikagundua kuwa bado ndani ya Tanzania tuna matatizo makubwa, hivyo inabidi tuyasolve kwanza matatizo ya ndani then tuangalie sasa tunatoboa vipi kimataifa.

Ndani ya Tanzania bado Tunamatatizo kibao, mfano;

MEDIA KUMILIKI WASANII.
Vyombo vya habari vya Bongo vimegawana wasanii, kuna wasanii wanasappotiwa na Media fulani, huku wengine wakisapportiwa na Media nyingine.

Sikuhizi kila media inawasanii wao, hasa hizi Media kubwa. So kama msanii haupo upande wa Media Fulani basi hautapata support, ili upate support lazima uwe chini yao na ukubali lolote watakalo kuomba.

Media zimesababisha matabaka makubwa sana baina ya wasanii, hivyo muziki hauwezi kwenda popote pale, Media ni lazima zisapport wasanii wote.

WASANII HAWASHIRIKIANI.
Tunaona kipindi Alikiba ametoa Album "Only One King" karibia kila msanii alipost Cover la Album hiyo, ila Harmonize alivyotoa album "High School" hakupata support yoyote kutoka kwa wasanii nje ya Konde Gang. Diamond hasupport kabisa wasanii wengine anachojua ni kussupport watu wa WCB tu.

WASANII HAWANA ELIMU
Wamekosa elimu ya muziki na Biashara ya Muziki. Wanaendaenda tu kwa uzoefu wakati sikuhizi Biashara ya muziki ipo kidigital zaidi na inahitaji watu Wajuzi sana. Bado wasanii hawajui faida ya kuwa na managers, kila kitu wanataka wafanye wao tu.

SUPPORT KUTOKA SERIKALINI
Serikali bado haijandaa sera ambazo zitainua zaidi muziki wa kitanzania, Imagine tuzo za muziki Zimesimama ndani ya miaka 6, ni aibu kubwa kwa nchi kama Tanzania kukosa tuzo.

Bado serikali haijaona umuhimu wa kuanzisha masomo ya sanaa Huko shule za msingi mpaka vyuo.

Tukisolve kwanza haya matatizo, basi kutoboa kimataifa itakuwa rahisi sana.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz