Msemaji Mpya wa Simba Afunguka Haya "Nimeamka Salama" - EDUSPORTSTZ

Latest

Msemaji Mpya wa Simba Afunguka Haya "Nimeamka Salama"



Afisa Habari wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally ameandika haya kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii:

Msemaji wa Mabingwa nimeamka salama Al hamdullillah🙏🙏

Awali ya yote nisema asante Wana Simba kwa mapokezi makubwa niliyopata kutoka kwenu hii ni ishara kuwa mnanipenda, mnaniamini na mmenikubali nami niwahakikishie tuu sintawaangusha.

Mapokezi yenu yamenipa nguvu, faraja na matumaini ya kuwa niko sehemu sahihi na sehemu salama, sehemu ya watu wenye upendo wa hali ya juu hakika hii sio timu hii ni Familia.

Nimepigiwa simu nyingi sana, nimepokea msg nyingi sana, zipo ambazo nimejibu na nyingi nimeshindwa kujibu naombeni mnisamehe kwa wote ambao nimeshindwa kupokea au kujibu msg zao.

Haina maana nimewadharau lakini kwa yoyote ambaye angependa tuwasiliane basi milango ya msemaji wenu ipo wazi muda wowote tuzungumzie Simba yetu.

Tuendelee kwa nguvu kuchangia Ujenzi wa Uwanja wetu, ndio ni lazima tujenge Uwanja wetu iwe jua iwe mvua.

Pia tuendelee kufuatilia mitandao ya kijamii ya timu yetu hakikisha mwana Simba una SimbaApp hakikisha ume Subscribe YouTube Channel yetu pamoja na ku follow page zetu za Instagram na Twitter...

Tushikamane tuna jukumu kubwa mbele yetu Ligi kuu ya NBC, Kombe la Azam Sports na Kombe la Shirikisho Africa tunahitaji kutimiza malengo ya Mashindano na Insha Allah tutafanikiwa

Mwisho kabisa tuendelee kuwaunga Mkono viongoz wetu tukianza na Rais wetu wa Heshima @moodewji ame dedicate maisha yake kwa Simba, anachohitaji kutoka kwetu ni kumuunga Mkono tu.

Pia Bodi ya Wakurugenzi Chini ya Mwenyekiti wetu @salim_tryagain @salim_abdallah_tryagain na Wajumbe wote wa Bodi ya Wakurugenzi wanafanya kazi kubwa kuijenga Simba wanachohitaji kutoka kwetu ni Sapport tuwe nyuma yao muda wote na tufuate maagizo yao.

Niseme tena Asanteni 🙏🙏 .





Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz