Mapenzi ya jinsia moja Kenya Kizungumkuti - EDUSPORTSTZ

Latest

Mapenzi ya jinsia moja Kenya KizungumkutiWaziri wa elimu nchini Kenya George Magoha ametoa tamko la kuzuiwa kwa wanafunzi wote ambao ni wapenzi wa jinsia moja kuhudhuria shule za bweni ili wasiwashawishi wanafunzi wengine.

Kulingana na Magoha, iwapo wanafunzi wanaovutiwa kimapenzi na wenzao wa jinsia wataruhusiwa katika shule za bweni huenda wakawashawishi  wanafunzi wengine kujiunga nao.

Magoha amesema badala yake wanafunzi hao wanapaswa kuhudhuria shule za kutwa zilizo karibu na makazi yao.

Magoha amependekeza kwamba wanafunzi kama hao ambao tayari wako katika shule za bweni wanapaswa kuhamishwa na kupelekwa katika shule za kutwa.


 
“Wajibu wako unapaswa kuwa kwa walio wengi zaidi na sio watu wachache. Usijiruhusu kutishwa na watoto” Magoha aliwaagiza walimu wakuu.

Suala hili limeibua gumzo nchini Kenya huku mashirika kadhaa ya kutetea haki za binadamu yakiapa kufika mahakamani kupinga utekelezaji wa agizo la waziri huyo.

Baadhi ya wanamitandao wamemuunga mkono waziri huku wengine wakimkashifu  kwa kile wanachosema ni  maoni ya kibaguzi dhidi ya wanafunzi wa jinsia moja.

Kwa mujibu wa Sheria za nchini Kenya mapenzi ya jinsia moja yanaweza kuadhibiwa kwa hadi miaka 14 jela ikiwa pingamizi kwa sheria hii ilikataliwa mwaka wa 2019.

Mwezi wa tisa mwaka 2021, bodi ya filamu nchini Kenya, KFCB, ilibainisha kuwa filamu ya “I am Samuel” haifai kuonyeshwa kwa umma kwani inasukuma hoja ya kuwa na ndoa za jinsia moja na kuzikubali kinyume na ibara ya 165 ya sheria ya filamu na uigizaji.

Ifahamike kuwa mapenzi ya jinsia moja ni marufuku katika mataifa mengi barani Afrika huku wataalamu wa afya wakisema wapenzi wa jinsia moja wanaongoza kwa maambukizi ya Ukimwi.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz