Card B Afunguka "Nilitaka Kujitoa Uhai Baada ya Muandishi wa Udaku Kudai Mimi ni Kahaba na Nina Magonjwa ya Zinaa" - EDUSPORTSTZ

Latest

Card B Afunguka "Nilitaka Kujitoa Uhai Baada ya Muandishi wa Udaku Kudai Mimi ni Kahaba na Nina Magonjwa ya Zinaa"Cardi B amefunguka kuhusu Kashfa nzito iliyoandikwa kuhusu yeye na mwandishi wa habari za Udaku Latasha kupelekea kutaka kuondoa uhai wake .

Cardi B alionekana katika mahakama ya huko Georgia Alhamisi asubuhi (Jan. 13) ili kutoa ushahidi katika kesi yake ya kashfa dhidi ya mwandishi wa habari za Udaku Latasha K Cardi aliangua kilio alipokuwa akieleza mahakama hali yake Baada ya kusikia habari hizo ambazo alidai ni za Uongo huku akidai alifikia hatua ya kutaka kujiua .
.
"Nilitaka kujiua kutokana na mambo hayo," alisema, kulingana na TMZ. Mapema mwaka wa 2019, Cardi alifungua kesi dhidi ya Tasha K, ambaye alichapisha mfululizo wa video akidai Cardi alikuwa kahaba na aliambukizwa magonjwa mengi ya zinaa. Katika video moja, Tasha alisema mtoto wa Cardi anaweza kuzaliwa na ulemavu wa akili, akisisitiza kwamba Cardi alikuwa akitumia dawa za kulevya wakati wa ujauzito wake .
.
Hii ilitokea muda mfupi baada ya Offset na Cardi kumkaribisha binti yao Kulture.
"Nilihisi kushindwa na kupatwa na huzuni na sikutaka kulala na mume wangu," alisema Cardi, na kuongeza kuwa alihisi kama "sikustahili mtoto wangu."
.
Wakili wa Cardi aliulizwa anafikiria nini kuhusu Tasha baada ya kuona video hizo.
"Nilihisi ni pepo pekee ndiye angeweza kufanya hivyo," alisema kabla ya kuomba msamaha kwa hakimu kwa kuapa mahakamani. Wakati moja kwa moj Instagram 2018, Cardi alitishia kumshtaki Tasha K kwa kueneza Uongo kuhusu yeye .

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz