Shaa na Master Jay Kinazidi Kuumana - EDUSPORTSTZ

Latest

Shaa na Master Jay Kinazidi Kuumana
MWANAMAMA wa kitambo kunako Bongo Fleva, Shaa, kupitia ukurasa wake wa Instagram amemtaka mzazi mwenzake, Producer Master J akamuone mtoto wake na kuacha kuposti picha za zamani mitandaoni, jambo linalotafsiriwa wawili hao wanazidi kuumana.

Shaa ameposti screenshot ya posti ya Master J na kuandika; “Unajua Nia (jina la mtoto wao) yupo wapi… mida yake..acha kuposti vitu vya nyuma…sijafunga mlango wa wewe kumuona.. infact..you still have a key… Nia angependa sana kurekodi chochote na wewe.. hujamuona kitambo.. umemposti..stop it…”

Wiki moja iliyopita Shaa aliweka ujumbe mrefu kunako Instagram kuhusiana na alivyoumia kwenye uhusiano wake wa kimapenzi kwa kupigwa na mpenzi wake na kufuta baada ya saa chache.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz