Mrembo Huddah Atangaza Kuuza Kizazi Chake, "Ukitaka Kuzaa na Mimi Weka Mzigo Bilioni Mbili" - EDUSPORTSTZ

Latest

Mrembo Huddah Atangaza Kuuza Kizazi Chake, "Ukitaka Kuzaa na Mimi Weka Mzigo Bilioni Mbili"


Mwanamitindo na mjasiriamali maarufu nchini Kenya Huddah Monroe ameweka wazi kuwa yuko tayari kuwa mama ikiwa mwanamume anayetamani kupata naye watoto ataweka mezani kitita cha $1,000, 000 ambazo ni sawa na zaidi ya Bilioni mbili za Kitanzania.

“Nauza tumbo langu. Lol! $1, 000, 000 ili niwe mama wa mtoto wako mchanga. Kuhusu Msaada wa mtoto tutakubalina wakati wa kushiriki tendo ili kupata mimba,” alisema Huddah Monroe.⁣
-
Mnamo mwaka 2020, Huddah alikiri kwamba kamwe hatoweza kumhifadhi kwenye tumbo lake mtoto wa mwanamume fukara,.

Kupitia kwenye Insta story yake, Huddah alisema kwamba katu, hatoweza kukubali kupata mtoto wa mwanamume asiye na uwezo wa kifedha kwa sababu hiyo ni sawa na kumleta mjinga hapa duniani hali ya kuwa unajua.

Licha ya kuweka hilo wazi pia alionesha kushangazwa na baadhi ya wanawake wanaokubali kushika mimba za wanaume wa namna hiyo. "Siwezi kuleta mjinga katika ulimwengu huu kwa kujua! Mungu aniepushie!"

@huddahthebosschick

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz