Hard Drive ya Marehemu 2Pac Shakur Inauzwa Bilioni 2.3 kwa pesa ya Tanzania - EDUSPORTSTZ

Latest

Hard Drive ya Marehemu 2Pac Shakur Inauzwa Bilioni 2.3 kwa pesa ya Tanzania


Ni takribani miaka 25 imepita tangu rappa 2Pac Shakur aiage dunia, alifariki mwaka 1996, na enzi za uhai wake album yake ya mwisho kuiachia ilikua ni "All eyes on Me" ambayo ilitoka Februari 1996.

Licha ya kwamba hatupo nae duniani, huenda hivi karibuni ukazipata kazi MPYA za rappa huyo.

Jana Jumatano imeingizwa sokoni Hard Drive iliyokuwa ikimilikiwa na 2Pac Shakur enzi za uhai wake, ni Hard Drive yenye uwezo wa GB 83, ikiwa ina kazi MPYA za kimuziki za rappa huyo kuanzia audio na video ambazo hakuwahi kuzitoa. Hard Drive hiyo imeingizwa sokoni kwa gharama ya Dola Milioni 1 ambazo ni takribani Bilioni 2.3 kwa pesa ya Tanzania.

Upo tayari kuinunua Hard Drive hiyo BILIONI 2.3?

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz