Diamond Platnumz Hajashuka Kimuziki...Usishangae hili goma likabamba na kubeba tuzo - EDUSPORTSTZ

Latest

Diamond Platnumz Hajashuka Kimuziki...Usishangae hili goma likabamba na kubeba tuzo



Mondi katoa ngoma inaitwa ‘Unachezaje’. Wabongo kama hawajaelewa. Wakiamini iko chini ya kiwango stahili cha ‘Mondi Bin Laden’ wao. ‘Komenti’ za huko ‘insta’ zitakupa picha kamili.

Tatizo ni kwamba ‘Mondi’ na Wabongo ni vitu viwili tofauti. Wabongo wanaamini Mondi ni mali yao na wanataka awalishe watakacho lakini kiuhalisia anatakiwa kuilisha dunia.

@diamondplatnumz mnayemtaka yupo kwenye ‘kolabo’ za kina #Zuchu. Kasikilize ‘vesi’ yake kwenye ‘Kwangwaru’ na Konde Boy. ‘Litawachoma’ au ‘Cheche’ na Zuchu. Yule ndiye Mondi wa Wabongo.

Mondi wa sasa hawezi kutoa wimbo kwa kuitazama Maneromango na Ubena Zomozi. Pengine hili ndo linafanya tusimuone Mondi yule wa ‘Ukimuona’ au ‘Mawazo’.

Mondi ni mali ya uso wa dunia hii. Vigumu kuimba kitu kama ‘Nitarejea’ na ‘Mbagala’ utegemee huko Gambia au visiwani Mayote wamuelewe.

Wa sasa ni wa midundo na mtiririko mtamu wa maneno. Hii hufanya hata asieelewa lugha basi afurahie midundo na ‘melodi’. Katika hili hahitaji kushikiwa bunduki kuelewa.

Note: Mtu ambaye miezi miwili iliyopita alikaa meza moja na #Snoop, #Busta Rhymes na #Swiss Beat,wizkhalifa. Wakijadili muziki halafu leo asijue ngoma ya kuachia?

Ukimtaka Mondi wa ‘Nenda Kamwambie’ na ‘Ukimuona’ subiri ‘kolabo’ yake na Linex ama Ben Pol, lakini ngoma zake binafsi kwa sasa ni kama ile ‘Parakatatumba’.

‘Kolabo’ yake na Davido ya ‘Number One remix’. Ilikuwa kama ‘roho kuacha mwili’. Kuanzia hapo mtazamo wake ulikuwa wa kidunia na siyo ‘Mongolandege’.

Usishangae hili goma likabamba na kubeba tuzo. Kwa sababu muziki wa dunia siyo ujumbe tu, bali ni kelele zilizopangiliwa vizuri…

Offer ya X Mass Tangaza Biashara yako yoyote Kwenye Blog Hii kwa Sh 10,000 tu

Piga simu 0714604974 kwa Maelezo zaidi






Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz