Zari Atoa Mpya "Sijawahi Rithi Chochote Kutoka Kwa Ivan" - EDUSPORTSTZ

Latest

Zari Atoa Mpya "Sijawahi Rithi Chochote Kutoka Kwa Ivan"Mwanamama Zarina Hassan maarufu Zari the bosslady amefunguka kuwa hakuwahi kurithi chochote kutoka kwa marehemu mumewe Ivan Ssemwanga aliyefariki mwaka 2017 na kuongeza kuwa walichokuwa nacho wote wawili walikifanyia kazi.

Zari amefunguka hayo kwenye episode ya kwanza ya kipindi kipya cha Talk with Toke Makinwa, cha mrembo Toke kutoka nchini Nigeria, “Tulipoungana tulikuwa na matamanio makubwa sana, nikimtazama alikuwa na uwezo mkubwa na aliponitazama aliona nguvu yangu.

Kwa hivyo tuliunganisha nguvu zetu zote mbili na kuunda himaya. Sijawahi kurithi chochote kutoka kwake. Kuna nyakati tuliendesha gari ambalo milango yake hata haikufunguka, lakini watu hawakujua hilo.

Lakini sasa mtu anapokuona unapost Lamborghini wanasema 'alirithi," - Alizungumza #Zari kwenye episode ya ufunguzi wa kipindi cha mrembo Toke Makinwa.

Sanjali na hilo, Mama huyo wa watoto watano amesema wakati mwingine yeye hutumia muda mwingi kulea na kuendesha biashara zake kiasi kwamba ni nadra sana kuwa na mwanamume.

Hata hivyo alieleza kuwa haimaanishi hataki kupendwa. "Nimechumbiana na watu kadhaa na wakati mwingine iliishia kutofanya kazi kwa sababu nilijitolea kwa kazi yangu na kwa watoto wangu. Nataka kutanguliza."

"Watoto wangu na biashara wananihitaji na lazima niamue wapi nitaweka nguvu zangu kwanza na ninapofanya baadhi ya wanaume wanadhani nina nguvu na kujitegemea. Wanawake wenye nguvu wanahitaji wanaume. Inakuwa vigumu kuchumbiana unapokuwa huru. Watu hufikiri, 'Ohh 'anazeeka na hahitaji mwanamume'." Alimalizia #Zari.

Na: @omaryramsey

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz