Spika wa Bunge, Job Ndugai Amewataka Wanawake Wenye Mamlaka Kutotumia Vyeo Vyao Vibaya - EDUSPORTSTZ

Latest

Spika wa Bunge, Job Ndugai Amewataka Wanawake Wenye Mamlaka Kutotumia Vyeo Vyao Vibaya

Spika wa bunge, Job Ndugai amewataka wanawake wenye mamlaka kutotumia vyeo vyao vibaya. Spika Ndugai amesema mtu akipewa mamlaka halafu akaanza kuvimba na kushurutisha kwa kuwaweka watu ndani kwani kunawaondolea sifa ya kuwa viongozi.


Ndugai ametoa kauli hiyo katika ukumbi wa Pius Msekwa bungeni alipokuwa akizindua mafunzo ya uongozi kwa wabunge wanawake. Mafunzo hayo yameandaliwa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) kwa lengo la kuwajengea uwezo wanawake katika uongozi.


Spika amesema Taifa linaloongozwa na mwanamke linakuwa tulivu , amani na salama. “Lakini kauli za baadhi zinaharibu taswira nzima, wengine mavazi yenu yanakuwa ya hovyo, ukipewa cheo kazi yako inakuwa ni kufoka na kuweka watu ndani jambo linaloharibu taswira ya viongozi wakuu wa nchi,” amesema Ndugai.


Amewaagiza wabunge wanawake kujifunza kwa bidii mafunzo hayo kwani ushahidi unaonyesha waliojifunza walibadilika na kuwa viongozi mahiri. Naye, Mwakilishi wa balozi wa Norway, Karen-Emilie Asla amesema mafunzo hayo ni kichocheo cha kumfanya mwanamke asijisikie mnyonge bali kila mtu anaweza kupewa nafasi.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz