Otile Acharuka "Zuchu & Mbosso Punguzeni Mazoea Mmeniibia Wimbo"





MSANII maarufu kutoka 254 nchini Kenya, Otile Brown amedai kuchukuliwa melody zake za wimbo wa ‘baby love’ kutumika kwenye wimbo mpya wa Mbosso na Zuchu uitwao ‘ #ForYourLove ‘.
Otile Brown ameweka taarifa hiyo kwenye page yake ya Instagram kwa kupost video ya wimbo wa Mbosso aliomshirikisha Zuchu kisha akaandika ujumbe ufuatao.
“Punguzeni mazoea basi, hiyo ni melody nzima ya #BabyLove , if you know you know, mna bahati sina utoto na roho mbaya…”
Video ya wimbo huo wa Mbosso na Zuchu imetoka leo na ina views 92,574 pia ipo trending namba 21 kwenye mtandao wa YouTube.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post