Jengo la Chuo cha Ulinzi lagharimu Bilioni 57 - EDUSPORTSTZ

Latest

Jengo la Chuo cha Ulinzi lagharimu Bilioni 57



 
Uzinduzi wa jengo jipya la Chuo Cha Taifa Cha Ulinzi Tanzania kilichopo Kunduchi mkoani Dar es Salaam, lililojengwa kwa msaada wa Jeshi la Ukombozi wa Watu wa China umefanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Rais Samia Suluhu, leo Novemba 14, 2021.
Akiongea kwenye uzinduzi huo Mkuu wa Majeshi Tanzania CDF Venance Mabeyo, amesema jengo hilo limegharimu shilingi Bilioni 57.

''Serikali ya China kupitia jeshi la ukombozi wa watu wa China, imetujengea jengo hili kwa msaada. Ujenzi wa jengo hili la kisasa lenye ghorofa 4 na nusu umegharimu shilingi bilioni 57'' - CDF Vanance Mabeyo.

Aidha ameongeza kuwa, ''Kufuatia jengo hili kukamilika chuo chetu sasa kinatarajia kuongeza nafasi za washiriki kutoka 40 hadi 100''.





Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz