Aliyekuwa Mke wa Halaki wa BEN Pol Afunguka "Sijutii Wala Kujilaumu Kuachana na Ben Pol Nina Mengi ya Kuzungumza ila Sitaki Kumdhalilisha" - EDUSPORTSTZ

Latest

Aliyekuwa Mke wa Halaki wa BEN Pol Afunguka "Sijutii Wala Kujilaumu Kuachana na Ben Pol Nina Mengi ya Kuzungumza ila Sitaki Kumdhalilisha"

 


Aliyewahi kuwa mke wa Msanii wa Bongo Fleva, Ben Pol aitwae Anerlisa yupo nchini Tanzania, amewasili Dar es Salaam muda mfupi uliopita na kufunguka mambo kadhaa ikiwemo ndoa yake na mkali huyo wa muziki.

Mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege (JNIA), @anerlisa alisema hataki kuzungumzia ndani kuhusu suala hilo la ndoa kwa kuwa analinda heshima yake na ya familia yake.

“Hutakiwi kuzungumzia ndoa, kwani siyo kama uhusiano wa kawaida, hata kanisani tuilifundisha hivyo, unatakiwa kuiheshimu,” alisema.

Alipoulizwa kama Ben Pol alikosea kuhusu kuzungumzia ndoa yao hadharani, alisema: “Ndiyo alikosea.

“Sitaki kuzungumza mengi kwa kuwa sitaki kudhalilisha nina Mengi Mno, wala sijutii kuachana naye kwa kuwa katika maisha kila kitu ni darasa.” 
.
.
.
#TimesFMDigital #TimesFmNiBaraka #HujasikiaBado #mgusowajamii📻🎧🎤🔥🔥🔥  
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz