Akaunti ya Benki ya Mwanafunzi wa Chuo Yakutwa na Bilioni 2.3, Serikali Yashtuka - EDUSPORTSTZ

Latest

Akaunti ya Benki ya Mwanafunzi wa Chuo Yakutwa na Bilioni 2.3, Serikali Yashtuka



Mahakama ya kupinga rushwa nchini Kenya imetoa amri ya benki kuzuia akaunti ya mwanafunzi Felesta Njoroge, ambaye ana umri wa miaka 21, hiyo ni baada ya kukutwa na salio la Sh bilioni 2.3.

Mamlaka ya Asset Recovery Agency (ARA) imezuia akaunti hiyo baada ya kugundua kuna wingi wa fedha katika akaunti hiyo wakati mhusika ni mwanafunzi.

Njoroge alipoulizwa juu ya fedha hizo ameeleza kuwa alitumiwa na mpenzi wake wa Ubelgiji, Marc De Mesel na kuambiwa kuwa anaweza kutumia kadiri anavyotaka.

Mamlaka imeagiza kuwa fedha hizo zizuiwe kwa muda wa siku 90 ili uchunguzi ufanyike.





Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz