Upanga wa miaka 900 wapatikana Israel - EDUSPORTSTZ

Latest

Upanga wa miaka 900 wapatikana Israel

 
Upanga unaoaminika kuwa wa mpiganaji wa zamani wa vita ya waasi takribani miaka 900 iliyopita umepatikana na mzama maji katika pwani iliyoko kaskazini mwa Israel.



Upanga huo wenye futi 3.3 uligunduliwa na Shlomi Katzin na kukabidhiwa na mamlaka.

Inadhaniwa kuwa upanga huo ambao ulikuwa baharini kwa muda mrefu umeonekana baada ya mchanga kuhama.

Mamlaka ya masuala ya kale nchini Israel (IAA) imesema upanga huo utakaposafishwa na kufanyiwa uchunguzi wa kina utawekwa katika maonesho ya umma.

“Upanga ambao umehifadhiwa katika hali nzuri , unavutia, ni uvumbuzi wa nadra na dhahiri kuwa ulikuwa wa shujaa wa vita,” alisema afisa wa kitengo cha uchunguzi cha IAA.

“Inafurahisha kukutana na kitu cha mtu kama hicho ambacho kinaturudisha miaka 900 iliyopita , wakati ambao silaha kubwa za kijeshi zilikuwa mapanga na visu”.

Wapiganaji waliopigana vita za kidini walifahamika kama ‘vita vya msalaba’ na vilihusisha kanisa katoliki.

Katika kampeni hizo, mashariki mwa bahari ya Mediterania wakilenga kugundua mji mtakatifu kutoka kwa utawala wa kiislamu.






Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz