Shilole, Alikiba Kimeumana! Una Kiburi cha Kishamba, Diamond Amekugaragaza - EDUSPORTSTZ

Latest

Shilole, Alikiba Kimeumana! Una Kiburi cha Kishamba, Diamond Amekugaragaza





KIMEUMANA… Hivyo ndivyo unavyoweza kusema! ni baada ya Supastaa wa Bongo Fleva, Alikiba kudai kwamba siku ya uzinduzi wa Albamu yake mpya ya ‘Only One King’ hakumwalika msanii mwenzake Shilole, hata yeye anashangaa alifikaje kwenye shughuli hiyo, Shilole ameamua kufyatuka mazima.

 

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Shilole ameandika kuwa: Hapana jamani, kila siku nakosewa nikitaka kuongea washauri wangu wanasema nikae kimya. HILI NIMEKOSEWA SANA NA SIWEZI KUKAA KIMYA SASA MNANIONEA. Alikiba nakushukuru sana leo umeuthibitishia ulimwengu mambo yafuatayo:

 

1. Una kiburi cha kishamba, unavimba na kupandisha mabega katika namna isiyostahili. Huna utu ambao watu wako wanakupamba kwamba uko nao. Sawa mimi na wewe hatuna mazoea (Hilo ni kweli kabisa), lakini mimi na wewe tupo katika field moja. Ningeweza kuja kwenye shughuli yako kuonesha upendo tu hata kama sijaalikwa, ungekuwa na utu, haikuwa na haja kwenda redio na kusema “SIJAMUALIKA” : ili mimi nionekane nilivamia tu shughuli tu? Shame on you Ali. (ila kwa tabia zile za kwenda Marekani kuomba dada zako naniliu hushangazi).

.
2. Umethibitisha kwamba wewe hauko ‘organized’. Kwa sababu, utasema nilipostiwa kwenye page yako na kutafutwa na watu wako wakati hawajakutaarifu. Kwa hiyo kwa ukubwa tunaotangaziwa unao Bwana Ali, unataka kusema hujui hata kilichopostiwa kwenye page yako rasmi katika siku yako muhimu? Kwa hiyo hata Nasibu uliyeshindana naye miaka mingi akakugaragaza angeweza kualikwa bila wewe kujua? (Nasibu humuwezi tusikudanganye). Wewe ndo msanii wetu wa kimataifa? SIJAPENDA.

Kwa ufupi, sikuenda kwenye shughuli kama mvamizi. Nilialikwa, nimescreenshot post yake na kupost hapo juu. Shughuli ile ya hovyo hovyo na kupoa kama uji wa mngonjwa, ilihitaji uwepo wangu. YEEES, Niliwasaidia kuchangamsha.

Katika mazingira ya sasa mimi hakuna lolote ninalofaidika kwa kwenda kwenye shughuli ya Ali, sana sana nilienda kumuongezea followers. Kama nahukumiwa, nihukumuni kwa kupenda shughuli za wenzangu. Kila nikialikwa Zuwena mimi nakweenda kuonesha upendo. NA SITAACHA KUFANYA HIVYO KWA SABABU YA WATU WALIOKOSA UTU NA SHUKRANI KAMA ALI




Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz