Sabaya Ambusu Mchumba Wake Kabla ya Kupelekwa Gerezani - EDUSPORTSTZ

Latest

Sabaya Ambusu Mchumba Wake Kabla ya Kupelekwa Gerezani
ALIYEKUWA Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya amembusu mchumba wake anayefahimika kwa jina la Jesca mara baada ya kuhukumiwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Arusha.

 

Sabaya na wenzake watatu wamehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha.

 

Akitoa hukumu hiyo jana Ijumaa Oktoba 15, 2021 Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Arusha, Odira Amworo amesema ameridhika kuwa upande wa mashtaka umethibitisha mashtaka dhidi ya Sabaya na wenzake pasi na shaka.

 

Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya hukumu hiyo, Wakili wa Sabaya na wenzake Mosses Mahuna amesema hawajaridhika na hukumu hiyo iliyotolewa kwa sababu ina upungufu mwingi.

 

Sabaya kabla ya kuhukumiwa aliiomba mahakama imuonee huruma na kumpunguzia adhabu kwanisi yeye bali alikuwa akitekeleza maelekezo kutoka kwa mamlaka za uteuzi wake huku akiieleza mahakama pia kwamba ana mhumba ambaye anatarajia kufunga naye ndoa na tayari ameshatoa mahari.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz