Rasmi mtandao wa Facebook wabadili jina lake na kuitwa Meta - EDUSPORTSTZ

Latest

Rasmi mtandao wa Facebook wabadili jina lake na kuitwa Meta 
Habari kubwa ni kwamba Mkurugenzi Mtendaji wa mtandao wa Facebook Mark Zuckerberg siku ya Alhamisi katika hafla ya kampuni yake ya Connect ametangaza jina jipya la Facebook na kuita Meta.


Mark Zuckerberg amesema kuwa “Leo tunaonekana kama kampuni ya mitandao ya kijamii lakini katika DNA yetu sisi ni kampuni inayounda teknolojia ya kuunganisha Watu ambapo Metaverse ni mstari unaofuata kama vile mitandao ya kijamii ilivyokuwa tulipoanza, jina hili limetokana na neno la Kigiriki meta ambalo linamaanisha ‘ZAIDI’ na kwangu mimi inaashiria kwamba daima kuna zaidi ya kujenga, hatimaye tunaweza kuweka watu katikati ya teknolojia yetu”


“Hii inatuonyesha na kutafakari kuwa sisi ni nani na tunatumai kujenga nini,” aliongeza. Alisema jina la Facebook halijumuishi kila kitu ambacho kampuni hiyo inafanya sasa, na bado linahusishwa kwa karibu na bidhaa yeyote, Lakini baada ya muda, natumai tunaonekana kama kampuni ya hali ya juu sana.”
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz