Muhamasishaji mpya wa klabu ya Simba @mwijaku_1 amegoma kufanya kile alichoahidi hivi karibuni mbele ya waandishi wa habari, kauli yake ya kwamba angetembea utupu bila nguo, endapo klabu yake ya simba ingepoteza katika mchezo wa marudiano wa klabu bingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana.
@mwijaku_1 ambaye pia ni mtangazaji wa kipindi cha Leo Tena cha Clouds Fm, akizungumza leo kwenye kipindi hicho amedai kwamba alikua tayari kutekeleleza ahadi yake lakini amejua kwamba sheria ya nchi haimruhusu kufanya hivyo.
Ikumbukwe klabu ya Simba imeondoshwa katika Ligi ya Mabingwa Afrika kwa msimu huu na Jwaneng Galaxy ya Botswana baada ya kuruhusu kufungwa bao 3-1 nyumbani kwenye mchezo wa jana jumapili katika dimba la Benjamin Mkapa.
Hayo yanajiri baada ya Simba kuruhusu kufungwa mabao matatu nyumbani na kufanya uwiano wa mabao kuwa 3-3 baada ya kushinda 2-0 ugenini hivyo wameondolewa kwa kanuni ya bao la ugenini.
Post a Comment