Harmonize Atoa Ahadi ya Kufanya Ngoma na 20 Percent, 20 Percent Afunguka Haya - EDUSPORTSTZ

Latest

Harmonize Atoa Ahadi ya Kufanya Ngoma na 20 Percent, 20 Percent Afunguka Haya

 


Hatimaye ahadi ya Teacher Konde @harmonize_tz ya kuingia studio na kufanya kolabo na @real_20percent pindi tu akitua kwenye ardhi ya Tanzania toka nchini Marekani imepokelewa kwa mikono miwili na mkali huyo wa zamani.

20 Percent ametumia insta story yake kumjibu Harmonize kuwa "Promise is like a debt" (ahadi ni kama deni) kwa maana yupo tayari hivyo Harmonize atimize alichokiahidi.

@real_20percent ambaye ni mshindi wa tuzo tano za Kili Music Awards 2010, aliwahi kutamba na ngoma kama Maisha ya Bongo, Mama Neema, Money Money, Tamaa Mbaya na nyingine kibao.


Majina ya Waliochaguliwa Kujiunga na Jeshi la Polisi, Names of Individuals Chosen to Join Tanzania Police Force

Haya yanajiri baada ya usiku wa kuamkia leo kuwa mrefu sana kwa @harmonize_tz ambaye alionekana akiburudika na midundo ya 20 Percent na kupelekea kutoa ahadi ya kufanya nae kolabo, sambamba na kueleza kuwa ni ndoto yake ya muda mrefu.






Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz